MAJUKUMU YA IDARA YA MIPANGO(WACHUMI)
1.Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii.
2.Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yatokanayo na utekelezaji wa sera za uchumi jumla
3.Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
4.Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi na maendeleo ya jamii.
5.Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa mbalimbali.
6.Kuainisha vipaumbele vya maendeleo.
7.Kuandaa ratiba ya kazi zinazohusika(action Plan)
8.Kutathmini na kuweka vipaumbele katika maeneo ya kuwekeza katika sekta za uzalishaji,miundombinu na maendeleo ya jamii na utawala.
9.Kutayarisha taarifa za mapitio ya mwenendo wa kiuchumi na kijamii za robo,na nusu mwaka
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa