IDARA Y A MAENDELEO YA JAMII
KAZI NA MAJUKUMU YA VITENGO
1.0 UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara kati ya Idara zilizopo Halmashauri Miji Kahama . Hii ni Idara mtambuka ambapo lengo lake kuu ni kuelimisha wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa (kuratibu upatikanaji, usambazaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali za Maendeleo). Kuhamasisha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kwa lengo la kujiletea maendeleo yao wao wenyewe. Idara hii inaamini kwamba maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe, ni imani yetu kwamba watu wanataka mabadiliko na wanaweza kubadilika, lakini hapa ifahamike kwamba mabadiliko yanayolengwa ni mabadiliko ya kimaendeleo na siyo vinginevyo. Kada ya Maendeleo ya Jamii inaamini katika falsafa ya Profesa Robert Chamber kwamba ”husimpe mtu samaki bali mfundishe mtu namna ya kuvua samaki”. Hii ikiwa na maana kwamba tuache kuwapa watu vitu/ kuwapelekea miradi ya maendeleo na badala yake miradi yote ya maendeleo itokane na wao wenye kwa njia shirikishi. Kwa utaratibu huu miradi yote ya maendeleo itakuwa endelevu.
Idara ya maendeleo ya jamii ina vitengo 6 kama vilivyoainishwa hapa chini, kila mkitengo na majukumu yake.
TAKWIMU NA MIPANGO
2. KITENGO CHA MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO.
3. KITENGO CHA MAENDELEO NA JINSIA
4. KITENGO CHA USTAWI WA JAMII
6. KITENGO CHA VIJANA
|
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa