Kwa kuzingatia umuhimu wa TEHAMA na lengo la serikali la kuwa na serikali mtandao, Halmashauri ya Mji Kahama ni miongoni mwa taasisi za serikali ambazo zinafanya vizuri katika eneo la TEHAMA.Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Mji wa Kahama ni ya kuridhisha kwa sasa.
Shughuli/Majukumu ya Kitengo
Kusimamia Mifumo yote tumizi katika Halmashauri
Kuweka na kusimamia miundo mbinu ya Mtandao Kiambo na intaneti
Kutoa msaada wa kiufundi kwa Watumiaji wa Miundo mbinu na vifaa vya TEHAMA
Kuandaa na kusimamia mifumo ya Usalama wa Kompyuta
Kusimamia utekelezaji wa shughuli kwa kutumia Serikali mtandaao
Kuandaa sera ya Matumizi ya taarifa za Kompyuta
Kusimamia Mifumo yote ya TEHAMA
Kuhakikisha teknolojia ya matumizi ya mifumo ya Kompyuta inaendana na wakati na ukuaji wa Teknolojia.
Kuandaa na kufanya tafiti na kupendekeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli ili kuboresha utoaji huduma kwa Halmashauri.
Kufanya Maboresho katika mifumo yote tumizi ya Halmashauri.
Kuandaa kituo cha utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya utunzaji taarifa za mifumo
Kusimamia na Kupitia vigezo vya mifumo na utoaji huduma
MAWASILIANO YA SIMU
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) ndiyo inayotoa huduma za mawasiliano ya njia ya simu katika ofisi zote za serikali na mashirika ya Serikali. Aidha Makampuni mengine ya simu za mkononi kama vile Vodacom,Tigo, Airtel, Halotel naZantel yametawanyika vizuri hadi vijijini na hivyo kufanya mawasiliano kuwa rahisi zaidi. Uwepo wa Makampuni mbalimbali umewasaidia wananchi kupata taarifa mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
VITUO VYA REDIO
Kutokana na mabadilko ya sera za habari na mawasiliano ambapo vituo binafsi vya radio vimeruhusiwa kuanzishwa, Mji wa Kahama sasa una vituo vitatu (3) vya radio. Vituo hivyo ni Kahama FM, Baloha FM na Divine FM.
MATUMIZI YA MIFUMO
Hadi kufikia Februari 2017 mifumo tumizi mbalimbali ya kisekta/kiidara imefungwa katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Kahama ili kurahisisha utendaji kazi na na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma. Mifumo hii ni pamoja na;
Mfumo wa Malipo (Epicor); Mfumo huu hutumika katika kuandaa na kutoa malipo. Mfumo huu umefungwa mwishoni mwa Januari 2017 na utasaidia sana kupunguza hoja za ukaguzi kwa kiwango kikubwa. Mfumo huu umeunganishwa kwa kutumia mkongo wa Taifa (fibre Optics)
PlanRep (Planning and Reporting) : Huu ni mfumo unaotumika kuandaa Mpango wa Bajeti na Kutoa taarifa. Mfumo huu wa PlanRep hutumiwa na Halmashauri wakati wa kuandaa bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
CDR na CFR--Hii ni mifumo inayotumika kutolea taarifa za miradi ya maendeleo katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Mfumo wa taarifa za Kiutumishi (HCMIS maarufu kama LAWSON): Huu ni mfumo unaotumika katika mishahara, kwa kutumia mfumo huu, serikali imeondoa tatizo la mishahara hewa, kuchelewa kwa stahili za watumishi n.k.
Mfumo wa Ukusanyaji Mapato (Local Government Revenue Collection Information System): Mfumo huu utumika katika shughuli za ukusanya wa Ushuru na Tozo mbalimbali za Halmashauri kwa Mujibu wa sheria.
Mfumo wa taarifa za Hospitali (Hospital Management Information System- GoT HOMIS): Mfumo huu hutumiwa na Hospitali kwa ajili ya kutunza taarifa za mbalimbali za Hospitali. Mfano, taarifa za Wagonjwa, Malipo, Dawa na Mengineyo. Kwa sasa mfumo huu umefungwa Hospitali ya Mji wa Kahama na Kituo cha Afya Mwenakulima. Maboresho yanaendelea ili uweze kufungwa katika Vituo na Zahanati zote za Halmashauri ya Mji.
HUDUMA YA INTANETI
Huduma ya intaneti Katika Halmashauri ya Mji hutolewa na makampuni mbalimbali. Kampuni ya simu ya TTCL ndiyo inayotoa huduma ya intaneti katika ofisi nyingi za serikali na mashirika. Aidha, makampuni ya simu za mikononi kama Vodacom, Tigo, Airtel na Zantel na halotel yanatoa huduma muhimu ya intaneti kupitia simu za mikononi na "moderm".
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa