• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

Utawala na Rasilimali Watu

Utangulizi:

Idara ya Utawala na Rasilimali Watu ni mhimili wa Uendeshaji wa shughuli za Taasisi hii za kila siku. Katika kutekeleza wajibu wake Idara inamsaidia Mtendajji Mkuu wa Halmashauri ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama. Aidha, Idara hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa Halmashauri  ina nyenzo za kutosha za kufanyia kazi, nyenzo hizo ni pamoja na rasilimali watu, fedha, majengo, usafiri, samani, n.k. Idara ya Utawala na Rasilimali Watu pia inao wajibu wa kuwezesha Idara zingine “Line Departments” kutenda kazi zake. Pia ina jukumu la kusimamia utendaji kazi katika Halmashauri kwa kuhakikisha kuwa malengo makuu ya Halmashauri yanafikiwa.

Idara ya Utawala na Raasilimali watu imegawanyhika katika sehemu kuuu mbili:-

Sehemu ya Utawala/Uendeshaji:

Kuhakikisha watumishi wanafuata Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma;

Kutafsiri Sheria na Kanuni za Utendaji kazi kwa watumishi katika eneo la kazi;

Kuhakikisha Ofisi  zina vitendea kazi vya kutosha;

Kusimamia utendaji wa Masijala ya Halmashauri

Kushughulikia masuala ya Itifaki;

Kusimamia Usafiri, Ulinzi na Usalama wa Majengo;

Kusimamia matengenezo ya vitemndea kazi vya Halmashauri.

Kusimamia ustawi wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni;

Kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na Rushwa;

Kuratibu Utekelezaji wa Mikakati ya Kuboresha Utendaji  katika Halmashauri;

Kushauri juu ya mbinu za kuongeza Ufanisi wa watumishi

Kuratibu Utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;

Sehemu ya Rasiliamali Watu:

1. Kuratibu Mafunzo- Idara inashughulika na kuratibu na kuandaa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi pamoja na kuandaa mafunzo ya awali ya watumishi. Utaratibu wa kwenda kwenye mafunzo hayo huanzia katika Idara husika baada ya mtumishi kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wake pamoja na elimu aliyonayo, Idara huamua kumuweka mtumishi katika bajeti ili aweze kuhudhuria masomo kulingana na mahitaji na mapungufu aliyonayo. Utaratibu huu unatokana na matokeo ya kujaza fomu za Opras ambapo changamoto za utendaji kazi huonekana katika fomu hizo.Hata hivyo Maombi ya kuingia kwenye mpango wa mafunzo yanaanzia Januari hadi Machi ya kila mwaka.

2.   Kuratibu Likizo – Idara inaratibu likizo zote za watumishi wa Halmashauri.
Watumishi wote wanatakiwa kujua kwamba likizo ni haki yao na ni muhimu kwao.Pia wanapaswa kujua kuwa utaratibu wa kwenda likizo huanzia kwenye Idara husika kwa Wakuu wa Idara kuandaa mzunguko wa likizo (Leave Roster) ya kila mtumishi kulingana na tarehe yake ya ajira . Pia wanapaswa kujua likizo za watumishi zinapitishwa kulingana na Leave Roster iliyowasilishwa. Aidha ijulikane pia kuna likizo ya malipo ambapo mtumishi anastahili nauli kwake na familia yake ikiwemo mke/mume,watoto wasiozidi wanne chini ya umri wa miaka18. Na iombwapo inatakiwa iwe na viambatanisho ambavyo ni cheti cha ndoa na vyeti vya kuzaliwa watoto na sio “Affidavit.”

3.         Upimaji Utendaji kazi wa wazi (OPRAS)- Idara pia inaratibu zoezi la Upimaji Utendaji kazi wa wazi yaani OPRAS kwa watumishi. Opras ni muhimu kwa watumishi kwenda kozi kwani ni kigezo kimojawapo cha upandaji cheo, na pia inaonyesha mapungufu ya Mtumishi kwa hitaji la kwenda masomoni, inaleta ufananisi katika kutekeleza majukumu, inaleta ushirikiano n.k. Zoezi la Opras hufanyika kila mwanzo wa mwaka wa Serikali yaani July ambapo watumishi wote wanatakiwa kujaza malengo yao ya mwaka katika fomu hizo baada ya kukubaliana na wasimamizi wao wa kazi. Aidha ifikapo Desemba wanatakiwa kufanya mapitio ya nusu mwaka wakieleza utekelezaji wa malengo yao ulipofikia na kama kuna mabadiliko yoyote ya malengo wanaweza kuyarekebisha hapa. Pia ifikapo mwisho wa mwaka yaani Juni kila mtumishi anatakiwa kueleza utekelezaji wa malengo aliyojiwekea mwanzo wa mwaka amefanikisha kwa kiwango gani halafu anatakiwa ajipime pia apimwe na msimamizi wake wa kazi. Kwa mwaka wa fedha 2015/16 watumishi zaidi ya 90% wamefanikisha kujaza fomu za Opras na wameanza kuelewa umuhimu wa fomu hizo.

4.  Mikopo ya Watumishi (1/3 ya Mshahara) Watumishi wanatakiwa kujua kwamba unapokopa unatakiwa ubaki na I/3 ya mshahara wako na kwamba mikopo yote inaingizwa kupitia system ya Lawson ili makato yaweze kukatwa kila mwezi.

5          Kushughulikia malimbikizo ya Watumishi Watumishi wote wanatakiwa kujua kuhusu utaratibu mpya wa malimbikizo (arrears). Mtumishi yeyote aliepanda cheo na akachelewa kurekebishiwa mshahara akawa na madai ya malimbikizo au ajira mpya aliechelewa kupata mshahara akawa anadai malimbikizo haitaji kujaza fomu za malimbikizo (arrears) kwa sababu kwa sasa malimbikizo (arrears) yanalipwa moja kwa moja. Hivyo anachotakiwa kufanya ni kwenda kwa Afisa Utumishi anaeshughulika na malimbikizo (arrears) na kuona kama madai yako yatalipwa moja kwa moja au kuna shida yeyote

6.         Kuratibu ajira, kuthibitisha kazini, kupandisha vyeo na uhamisho wa watumishi;

7.         Kuandaa Mpango wa Rasilimali Watu wa Wizara na mahitaji ya Wataalamu wa Wizara;

  • Usimamizi na uendesheaji wa masuala ya Mishahara;
  • Kushughulikia stahili mbalimbali za watumishi;
  • Kushughulikia stahili za watumishi wanapostaafu kazi ama kuacha kazi.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO January 01, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    May 14, 2025
  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa