Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa kuanzia Tarehe 1/3/2020 watumishi wote wa Umma ni lazima waishi karibu na maeneo yao ya kazi. Ametoa agizo hilo mapema leo alipofanya kikao na Watumishi wa Umma waliopo Kata ya Nyandekwa.
"Haiwezekani mtu afundishe Chalya halafu anaishi mjini, nguvu anayoitumia kwenda shule hawezi kufundisha kwa ufanisi, hivyo naagiza kufikia Machi 1 mwaka huu kila mtumishi aishi karibu na eneo lake la kazi. Nitavumilia iwapo utaniambia unakaa Katani lakini sio nje ya Kata". Amesema Msumba.
Msumba yupo kwenye ziara ya kutembelea Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kahama na kufanya vikao na Watumishi wa Uma, viongozi na kamati za Maendeleo ya Kata lengo likiwa ni kujionea na kusikiliza changamoto na kuzipatia suluhu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa