Mkurugenzi wa Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba mapema leo amefungua Mafunzo kwa Wataalamu wa Mji wa Kahama ngazi ya Kata juu ya Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo "O&OD" ulioboreshwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katika mafunzo hayo wataalamu hao wamesisitizwa kushirikisha jamii katika kila hatua ya maendeleo ikiwemo uibuaji wa miradi ya vipaumbele ili kuwezesha bajeti ya Halmashauri kumgusa kila mtu katika jamii.
Mfumo ulioboreshwa wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo unamtaka mwananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo Uibuaji wa Miradi ya vipaumbele, Kuweka jitihada zao kwenye miradi hiyo mfano uchangiaji wa rasilimali fedha, vifaa na nguvu kazi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa