Wataalamu na Viongozi wa Halmashauri ya Mji Kahama wapewa Mafunzo juu ya Mfumo Mpya wa Ruzuku ya Maendeleo Ulioboreshwa. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na uelewa viongozi na wataalamu wa Mji wa Kahama juu ya malengo na utendaji kazi wa Mfumo huu ulioboreshwa.
Mgeni rasmi Katika Mafunzo haya, Kaimu Afisa Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ndg. Alphonce Benedict Kasanyi ametoa mada ya Misingi ya utawala bora ambapo amebainisha misingi kadhaa ikiwemo Ushirikishwaji, usikivu, haki na umoja, uwajibikaji, ukweli na uwazi, utawala wa kisheria, Weledi, Uadilifu na Heshima kwa watu,
Akiwasilisha mada ya mfumo huo, Mwezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bi.Tatu Lesso amesema kuwa mfumo huu ulioboreshwa una lengo la kushirikisha jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili kadri inavyowezekana.
Aidha Bi. Tatu ameongeza kuwa katika mfumo huu serikali yapaswa kutambua umuhimu wa jitihada za Kijamii (Community Initiatives) na kuwezesha maeneo yenye mapungufu ili kufikia kutoa huduma bora na iliyolengwa kwa wananchi.
Mafunzo yameanza Ijumaa Tarehe12/05/2017 na kutarajiwa kuisha Jumamosi ya Tarehe 20/05/2017 ambapo mafunzo yanatolewa kwa wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji/Mitaa, Wataalamu wote ngazi ya kata na vijiji/mitaa, Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa na Waheshimiwa Madiwani.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa