Wanawake wa Mji wa Kahama wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda miti kuzunguka kituo cha afya Iyenze kilichopo Kata ya Iyenze Wilayani Kahama. Zaidi ya miche elfu mbili ya miti ya Matunda imepandwa katika eneo hilo.
Akiongea katika maadhimisho hayo, Kaimu mkurugenzi wa Mji wa Kahama Ndg. Robert Kwela amewaasa wananchi kuitunza hiyo miti ili iweze kuleta mvuto na kutunza mazingira. Siku ya Wanawake huadhimishwa tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka. Kauli mbiu ya Siku ya wanawake mwaka huu inasema kuwa "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa