Taharuki na hali isiyo ya kawaida imejitokeza jana katika mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga Mjini Kahama baada ya wananchi kufurika na kuanza kuchimba wakiamini kuwa eneo hilo lina madini ya Dhahabu.
Haijaeleweka mara moja nani aliyeanzisha mchakato huo na kuwaaminisha wananchi uwepo wa madini hayo katika eneo hilo. Hata hivyo jeshi la polisi lilifanikiwa kuwatawanya watu hao na kufanya hali ya amani kurejea.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Fadhili Nkurlu amewaonya watu wote kutoendesha zoezi la uchimbaji katika eneo hilo kwani suala la madini lina Mamlaka yake na taratibu zake.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa