Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imeendelea kuwa Halmashauri ya Mfano katika masuala ya Uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu alipokua akitoa sababu ya kwanini Mkutano wa Tathmini ya Lishe umeletwa kufanyika Kahama.
Katika Mkutano huo ambao umejumuisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala Mkoa, Waganga Wakuu wa Mikoa na maafisa Lishe nchi nzima uliofanyika Manispaa ya Kahama umewapa Fursa viongozi hao kutembelea maeneo mbalimbali ya Uwekezaji ndani ya Manispaa hii.
Wakiwa katika ziara hiyo wakuu wa mikoa wameahidi kwenda kufanya yale walioyaona kwenye Mikoa yao na kuahidi kuwa watafanya vyema zaidi ya waanzilishi (Kahama).
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa