Wakulima wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wamenufaika na Pembejeo za Kilimo za ruzuku zilizogawiwa na Halmashauri hiyo mapema leo.
Akiongea wakati wa kukabidhi pembejeo hizo Mkurugenzi wa Mji wa Kahama Ndg Anderson Msumba amesema kuwa ruzuku hiyo inatolewa ikiwa ni njia moja wapo ya kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.
Halmashauri ya Mjivwa Kahama kwa mwaka huu wa fedha imetenga milioni sabini na mbili (72) kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo zitakazogawiwa kwa vijana watakaojitokeza kulima kuanzia ekari tano za mazao ya biashara au chakula.
Kwenye pembejeo zilizogawiwa leo zimegharimu Jumla ya Tsh. 24,850,000.
Wanufaika waliojitokeza na kupewa pembejeo ni 545 Kwa matarajio ya ekari 725 zitakazolimwa. Ambapo Mtama Ekari 500, Mpunga ekari 125, Mahindi 75, Alizeti 15 na Pamba ekari 10.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa