Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kimefanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama huku waalikwa wakifunguka katika kuhoji na kushauri masuala ya maendeleo ya Wilaya. Kubwa lililohojiwa na wadau wengi ni wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA). Imeonekana kuwa watu wengi walikuwa hawaelewi TARURA ni nini na inafanyaje kazi. Mameneja wa TARURA wa Halmashauri za Kahama wameweza kuelezea kikao majukumu yao na mipango waliojiwekea.
Kikao kimeongozwa na Mwenyekiti Mhe. Fadhili Nkurlu, Mkuu wa Wilaya ya Kahama. Agenda kuu zilikuwa ni
1. Kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 na mpango wa bajeti 2018/2019 kwa Halmashauri zote 3 za Kahama i.e Ushetu, Msalala na Kahama Mji.
2. Mpango wa kuwarasimisha wafanyabiashara ndogndogo Wilayani Kahama
3. Umuhimu wa waajiri kutekeleza sheria ya "hifadhi ya mifuko ya jamii" kwa kuwasilisha michango ya watumishi wao kwa wakati.
Wajumbe wa kikao hiki ni Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya, Wakuu wa idara na vitengo Halmashauri zote 3, Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri zote 3, viongozi wa taasisi na wadau mbalimbali wa Wilaya.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa