Wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu Mjini Kahama wameonesha kutofurahishwa na aina ya teknolojia wanayotumia katika shughuli zao.
Hayo yamebainishwa na wachimbaji wa mgodi wa Mwime Wilayani hapa walipotembelewa na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mapema Leo.
"Tumekuwa tunatumia teknolojia ya kizamani Sana na wakati mwingine tunatumia hata waganga wa kienyeji kubashiri maeneo yenye Mali, tunaiomba serikali itufikirie kutupatia vifaa vya kisasa na watafiti wa miamba ili irahisishe utendaji wetu wa kazi" Alisema mmoja wa wachimbaji.
Akijibu maombi ya wachimbaji hao, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amewaahidi wachimbaji hao kuyafikisha na kuishauri serikali juu ya Yale waliyoomba.
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kukagua Miradi ya Afya, Uvuvi,mazingira, Vijana na Wanawake inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa