Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. Kangi Lugola leo amefanya ziara Halmashauri ya Mji Kahama ambapo jambo kubwa alilolikazia ni suala zima la uhifadhi wa Mazingira. Mh. Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama kusimamia upandaji miti kama ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoagiza.
Aidha Mh. Lugola amewaasa wananchi kujizoesha kutumia nishati mbadala kama vile gesi na majiko ya udongo badala ya kutumia kuni ambazo zinachangia uharibifu na ukataji wa miti.
Aidha Naibu Waziri ameoneshwa kutofurahishwa na tabia ya wachimbaji madini wadogowadogo ya kukata miti na kuitumia kama nyenzo zao na kutumia zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu, amewataka wachimbaji hao kutumia njia na teknolojia za kisasa katika shughuli zao ili kudumisha uhai wa mazingira.
Katika hatua nyingine Mh. Lugola amempa siku mbili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama kutoa Maelezo kwa maandishi katika Ofisi yake Kwanini hakulipa faini aliyopigwa kama adhabu kwa kutokidhi vigezo vya ki mazingira kipindi cha ziara ya aliyekuwa Naibu waziri Luhaga Mpina.
Mh. Naibu waziri ameahidi kurudi Kahama na kuanza ukaguzi wa maeneo yaliyopandwa miti mwezi Januari.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa