Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wamefika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa lengo la kujifunza namna Halmashauri hiyo inavyotekeleza Miradi ya Maendeleo, Uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi na Matumizi ya asilimia kumi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu. Wakiwa Kahama viongozi hao wametembelea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Viwanda "Ummy Mwalimu Industrial Park", pia wamefika eneo la CDT ambalo ni eneo rasmi kwa Wamachinga na kujionea 'Show room' ya samani ya mjasiriamali aliyewezeshwa na Manispaa ya Kahama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa