Maafisa wawezeshaji wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Kahama wametakiwa kuwa waadilifu wakati wa zoezi la uhakiki wa Kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo na Wawezeshaji wa TASAF juu ya utekelezaji wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF .
Msumba amewataka wawezeshaji hao kuwa makini wakati wa mafunzo ili kufanikisha zoezi la uhakiki wa kaya za walengwa wa TASAF na kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya kuwepo Walengwa hewa.
Aidha, Msumba amewataka wawezeshaji hao ambao ni watumishi wa Umma kuwa waaminifu na waadilifu wakati wa zoezi hilo.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Mafunzo na Ushirikishwaji kutoka TASAF Makao makuu,Ndg.MERCY MANDAWA amesema wawezeshaji kwenye Halmashuri zote nchini wamechangia kwa kiasi kikubwa katiks utekelezaji wa TASAF kuwa rahisi ,hivyo ametoa rai kwao kutumia mafunzo hayo kuisaidia jamii kujua kutunza kumbukumbu na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kutoka hali duni.
Semina hiyo ya kuwajengea uwezo Wawezeshaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama inafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 20 hadi 21,Julai 2020.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa