Halmashauri ya Mji wa Kahama imekabidhi rasmi eneo linalotakiwa kujengwa Hospitali ya Kisasa kwa Suma JKT ambao ndio watakaojenga majengo hayo. Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo kati ya Mkurugenzi wa Mji wa Kahama na Mhandisi wa Suma JKT.
Akipokea eneo hilo Mhandisi wa Suma JKT 'Major' Onesmo Njau ameahidi kuwa ujenzi utaenda kuanza mapema iwezekanavyo.
Suma JKT ndio ilishinda zabuni ya Kujenga hospitali ya Mji wa Kahama na Tarehe 29.08.2018 ilitia Saini Mkataba wa ujenzi huo.
Ujenzi huu ambao kwa awamu ya kwanza unaanza na jengo la OPD unatarajiwa kugharimu Shilingi za ki-Tanzania Bilioni 3.2 na unatarajiwa kukamilika Miezi 18 baada ya tarehe ya kuanza ujenzi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa