Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeitaka jamii kuwajibika katika kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu. Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru Halmashauri ya Mji wa Kahama jana tarehe 23.08.2018.
"..jamii tunawajibu wa kuwekeza katika elimu, kwa kuweza kuchanga fedha au kutumia nguvu kazi zetu sisi wenyewe kuweza kujenga miundombinu hii, lakini katika upande wa uchangishaji wa fedha Serikali imetoa utaratibu, kamati inayotakiwa ihusike katika uchangishaji wa fedha hasa katika ujenzi wa miundombinu ni Kamati ya Maendeleo ya Kata au Kamati ya Maendeleo ya Kijiji. Na kamati hizi zinachaguliwa na wazazi wenyewe katika vikao ambavyo ni rasmi na mkiwachagua watu hawa wajibu wao ni kuhakikisha kwamba wanasimamia maendeleo ya sehemu yenu hasa katika upande wa ujenzi wa miundombinu" Amesema Ndg. Kabeho.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwanunulia vifaa vya shule watoto zao na kuchangia chakula kwa wanafunzi ili kupunguza utoro mashuleni.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa