Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeziagiza Halmashauri ambazo bado hazijakamilisha ujenzi wa Maabara za masomo ya Sayansi "fizikia, kemia na Baiolojia" kuendelea na ukamilishaji huo. Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru eneo la Kagongwa Halmashauri ya Mji wa Kahama siku ya jana tarehe 23.08.2018.
"Lakini pia Serikali imeagiza, ndugu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, katika halmashauri yako ya Mji kama bado kuna sekondari ambazo hazijakamilisha ujenzi wa maabara tatu, maabara ya Fizikia, Kemia pamoja na Baiolojia endeleeni na ujenzi wa maabara hizi, lengo la serikali vijana wote wanaosoma masomo ya sayansi waweze kusoma masomo haya kwa njia ya vitendo" Amesema Ndg. Kabeho.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa