Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children leo limetoa vifaa vya Ofisi katika kituo cha huduma mjumuisho kilichopo Halmashauri ya Mji Kahama. Akikabidhi vifaa hivyo Mratibu wa masuala ya Ulinzi wa mtoto wa Taasisi hiyo Bw. Alex Enock, amesema kuwa wao wanalengo la kuona kuwa huduma kwa mtoto inaboreshwa, hivyo kwa kutumia vifaa hivyo kituo hiko kinaweza kuwa sehemu nzuri ya kutolea huduma. Vifaa vilivyokabdidhiwa ni pamoja na Runinga moja, Kabati moja, Viti viwili, Meza mbili, Kitanda cha wagonjwa kimoja, na Midoli ya kuchezea watoto.
Akipokea vifaa hivyo kwaniaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama, Mganga Mkuu Dkt. Lucas Ngamtwa amelishukuru shirika hilo kwa kujitoa kwake katika kuhakikisha usalama wa mtoto unakuwepo. Aidha ameahidi kutumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa