Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Ndg. Joseph Nyamhanga ameimwagia sifa Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kiwango cha juu. Amezitoa sifa hizo mapema leo alipokuwa akikagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
"Niwapongeze Kahama kwa kazi nzuri mnazozifanya, mmeweza kutumia mapato yenu ya ndani kujenga jengo hili kubwa la hospitali bilioni tatu nukta mbili, pia nimeona jengo mnalojenga la utawala mnatumia milioni mia tisa na kitu pia ni mapato yenu ya ndani, nadhani wengine waje kujifunza kupitia halmashauri ya Mji wa Kahama. Unajua Halmashauri ya Mji wa Kahama inapaswa kuwa na jengo linaloendana na hadhi yake, na naona nia yenu" amesema Nyamhanga.
Miradi aliyoitembelea Katibu mkuu ni pamoja na Ujenzi wa jengo la Utawala, jengo la hospitali ya Mji wa Kahama, ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Nyasubi, eneo la Viwanda Chapulwa na eneo la Viwanda Bukondamoyo "Dodoma".
Katibu Mkuu amepita Kahama ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya kazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa