Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mhe. Sindano Machum amewataka Wananchi wa Manispaa hiyo kujitokeza Kulipia ankara za malipo "Control Number" walizopatiwa kwaajili ya Kuandaliwa Hati Miliki za Ardhi zao.
Ametoa rai hiyo jana alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi ya Mtaa wa Mwime Kata ya Mwendakulima ambapo imeripotiwa kuwa kuna idadi kubwa ya Wananchi waliopatiwa Ankara za Kulipia Hati lakini bado hawajalipia.
Akitoa Taarifa kwa Mgeni Rasmi Bw. Mashili Mashili ambaye ni Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa hiyo amesema kuwa zaidi ya Watu elfu nne wametuma maombi ya kuandaliwa hati lakini waliofanya Malipo baada ya kupatiwa ankara ni asilimia mbili tu.
Aidha Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Shinyanga Ndg. Leo Komba ameainisha faida za kuwa na Hati Miliki ikiwa ni pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi na kuweza kuaminika na taasisi mbalimbali zikiwemo za fedha.
Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Kwa Manispaa ya Kahama Bw. Ladyslaus Munwingili amewataka wananchi wa Manispaa hiyo kuendelea kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa kuomba kuandaliwa Hati miliki na kuwasiliana na dawati la msaada la Manispaa ya Kahama mara kwa mara wapatapo changamoto.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa