Mwenge wa Uhuru 2017 katika Halmashauri ya Mji Kahama umepokelewa leo tarehe 15/07/2017,Ukiwa Halmashauri ya Mji Kahama, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa Km 55.8, katika Kata 13, vijiji 2 na mitaa 18 umepitia jumla ya miradi 12 , yenye thamani ya shilingi 6,956,951,494. Ambapo umeweka mawe ya msingi miradi 3 yenye thamani ya shilingi 721,410,000,umezindua miradi 3 yenye thamani ya shilingi 799,664,605, kufungua miradi 3 yenye thamani ya shilingi 268,198,089 na kukagua shughuli/bidhaa miradi 3 yenye thamani ya shilingi 5,167,678,800.Miradi hii ni ya sekta za elimu, Afya, Maji, Barabara, hifadhi ya mazingira, vijana wajasiriamali ,wanawake, mapambano dhidi ya UKIMWI, mapambano dhidi ya malaria, rushwa na madawa ya kulevya.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa