Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewaonya wafanyabishara ndogondogo kutokubali kuwa mawakala wa Wafanya biashara wakubwa katika matumizi ya Vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo. Ameyasema hayo mapema leo katika tukio la ufunguzi wa ugawaji wa Vitambulisho kwa Wafanyabiashara ndogondogo lililo fanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Wilayani hapa.
"Hivi ni vitambulisho vya Wafanya biashara ndogo ndogo na sio vitambulisho vya Wafanya biashara wadogo..naomba tuelewane kwa hilo, Wafanya biashara ndogo ndogo ni wale ambao wanafanya biashara ambayo mapato yake ghafi sio zaidi ya milioni nne kwa Mwaka, na tumesikia kuna wafanyabiashara wakubwa wamewaambia watu waende kuchukua vitambulisho ili wawatumie kuuza bidhaa zao mtaani, kwa hili niwaombe wafanya biashara ndogondogo msije kwenda kuwa mawakala wa hao wafanya biashara, Ukikakutwa unafanya hivyo utakamatwa na utachukuliwa hatua". Amesema Macha.
Mhe. Macha amesema kuwa Kwa Wilaya ya Kahama kwa awamu ya kwanza imepokea vitambulisho elfu kumi na vitagawiwa kwa wafanyabiashara ndogo ndogo ambao watakuwa wamekidhi vigezo. Vitambulisho vitagaharimu shilingi elfu Ishirini kwa mtu mmoja.
Aidha kwa upande wa wafanyabiashara wameonekana kulipokea vizuri zoezi hili na wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu.
Fomu zitaendelea kutolewa katika ofisi za Kata na Halmashauri kwa muda wa kazi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa