Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewaasa Wanachi wa Wilaya hiyo kukata Bima ya Afya ya Jamii ya CHF iliyoboreshwa kabla hawajaugua kwani hawajui Muda watakaokutwa na matatizo.
Ameyasema hayo Jioni ya leo alipokuwa akiongea na Wananchi wa Mtaa wa Shunu kwenye mkutano wa hadhara.
"Watu wanadhani huduma za afya ni dawa tu wanazo tafuna,
Kuna mambo ambayo watu wanayabeza mwanzoni lakini mwishoni ndo wanajua kuwa ni kimbilio.
Matibabu sio dawa tu, matibabu yanaanzia mapokezi ambapo unatakiwa kutoa hela, Vipimo vinahitaji hela, na dawa zina hitaji hela. Anzeni kukata Bima kabla hamjaugua" Amesema Macha.
Aidha Mhe. Macha aesema kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama inaendelea na uratibu wa kuwapatia Bima za Afya Wazee lakini amebainisha kuwa wazee wenye uwezo wa kujimudu ni vyema wanunue bima yao binafsi ili wengine wasio na uwezo wapate fursa.
Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa kwasasa ni Shilingi elfu thelathini na inahudumia Kaya ya watu sita kwa Mwaka Mmoja ikiwa ni sawa na elfu tano kwa mtu mmoja kwa mwaka.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa