Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ameelekeza kuachiwa huru kwa Wafanyabiashara wawili wa Matunda walioshikiliwa kwa kosa la kushambulia askari wa Manispaa ya kahama waliokua wakitimiza wajibu wao.
Ametoa msamaha huo mapema leo alipotembelea na kuongea na wajasiriamali wa Soko la Matunda na Machinga lililopo Eneo la CDT Mjini Kahama.
"Nimetoa msamaha kwenu ili iwe funzo kwenu na kuwapa nafasi ya kujirekebisha, serikali ina malengo makubwa kwa vijana.. Serikali inataka muwe pamoja, muunde vikundi vingi ili kama hamna mitaji iwakopeshe, na mikopo inayotolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan haina ubaguzi wa wa itikadi za vyama, uwe Chadema, iwe CUF, NCCR au CCM wote ni wa Tanzania, ni marufuku kwa machinga kufilisika.. " Amesema Kiswaga.
Mhe. Kiswaga amesema Ziara yake kwenye eneo hilo imetokana na kuona kipande cha Video kilichokuwa kinasambaa mitandaoni kikionesha Mgambo wa Manispaa ya Kahama wakibeba bidhaa za muuza matunda aliyekua akifanya biashara pembezoni mwa barabara.
"Unajua mitandao ya Kijamii ina nguvu sana, na jambo linasambaa kwa haraka sana kupitia mitandao hiyo, nlipoona hiyo video hiyo nikawasaliana na viongozi lakini sijaridhishwa na maelezo yao na ndio maan nimekuja hapa, ila kwa maelezo ya Mheshimiwa Diwani na viongozi wa Machinga nimejiridhisha kuwa Wale vijana walikua na makosa, ila tunawapa nafasi nyingine..na nakuagiza kiongozi wa eneo hili kuwapatia hawa eneo la kufanyia biashara zao ndani ya eneo hili ambalo lipo rasmi kwa kazi hiyo..na Mkurugenzi ameweka wazi kuwa ikifika saa moja jioni mnaruhusiwa kwenda huko barabarani lakini asubuhi na mchana eneo la biashara ni hili.." Amesema Kiswaga.
Katika hatilua nyingine Mhe. Kiswaga amewaasa askari wa Manispaa kufanya jukumu lao la msingi la Kulinda wafanyabiashara wafanye biashara kwa amani badala ya kuwabughudhi na kuwapa hofu na inapotokea changamoto kabla hawajachukua hatua wawasiliane na viongozi kwanza.
Kwa upande wao wafanyabiashara hao waliokumbwa na hiyo kadhia wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa Msamaha na wameahidi kutii na kufuata sheria zilizowekwa na Serikali.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa