Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack leo amehitimisha ziara yake Wilayani Kahama kwa kukagua Maendeleo ya Kilimo Halmashauri ya Mji Kahama. Akiwa Mji wa Kahama Mkuu wa Mkoa ametembelea mashamba na kuongea na wakulima moja kwa moja. Bi. Tellack amewaagiza maafisa Kilimo kuendelea kuwafikia wakulima na kuwashauri.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na hali za mazao mashambani na kuwaasa wakulima kukumbuka kuweka akiba pindi wakivuna mazao yao.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama Ndg. Anderson Msumba ameahidi kumsaidia Mkulima wa Pamba wa kijiji cha Ngulu kata ya Ngogwa Ndg. Richard Mifuko 48 ya Mbolea na Bomba la kupulizia dawa baada ya kuvutiwa na jitihada za mkulima huyo ambaye amelima ekari 24 za zao la Pamba.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa