Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Zainab Telack ameahidi kuchangia bati tisini (90) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati Mtaa wa Mhungula Mjini Kahama iwapo wanachi watajitolea kujenga boma. Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Mhungula Mjini Kahama Mapema leo. Mh. Telack amewaomba wananchi kuendelea kujitoa katika masuala mazima ya Ujenzi wa Miundombinu ya kutolea huduma za Jamii.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama Ndg. Anderson D. Msumba amewahakikishia wakazi hao kuwa iwapo watafikisha jengo hatua ya 'renta' atamalizia na kununua vifaa na kuleta watumishi kuanza kazi kufikia Juni mwaka huu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa