Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba, leo amefungua mafunzo ya OPRAS iliyoboreshwa kwa Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu na Wakuu wa Shule yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Akiongea katika Ufunguzi huo Msumba amewasisitiza washiriki kuwa makini kiasi cha kutosha kuelewa vizuri maana, matumizi na umuhimu wa OPRAS ikizingatiwa kuwa OPRAS sahihi ndiyo kigezo pekee cha kisheria katika kutambua na kutathmini utendaji kazi wa kila mtumishi wa Umma, na hivyo kuwezesha siyo Tuzo tu bali na Tozo pia.
Aidha amewaasa kuwa wakifanya kazi kwa bidii kwa kujiamini, kwa kuzingatia weledi, Sheria, taratibu na kanuni hakuna yeyote atakayeweza kuwanyima haki au stahili bila sababu ya msingi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa