Kamati ya Bunge ya Usimamizi wa hesabu za Serikali za Mitaa mapema leo imetembelea miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama na kupongeza hatua iliyofikiwa na Mji wa Kahama kwa ubunifu wa matumizi ya fedha za asilimia kumi za Wanawake, Vijana na Walemavu.
Pongezi hizo zimekuja baada ya Kamati hiyo kujionea eneo kubwa lililotengwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa ajili ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Katika eneo hilo wafanya biashara wamepatiwa maeneo bure ili kuendeleza biashara zao na pia Halmashauri imewaunganisha wafanya biashara hao na kuanzisha SACCOS yao ambayo Halmashauri inaenda kuwapatia Milioni mia moja kama mtaji.
Kamati ikiwa Kahama imetembelea eneo la ujenzi wa jengo la Hospitali ya Mji wa Kahama, Eneo la Ujenzi wa bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Abdurahim Busoka na eneo la Viwanda Bukondamoyo maarufu kama Dodoma.
Katika maeneo ya ujenzi Kamati imeshuhudia kazi zinazoendelea na imeshauri pale ilipoona kuna haja ili kuboresha ubora na ufanisi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa