Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mapema leo wamepatiwa mafunzo ya utendaji kazi wa nafasi zao kwenye Mamlaka za Serikali za Mtaa.
Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili Mkuu wa wilaya ya kahama Mhe. Anamringi Macha amewaasa madiwani kuwa makini kusikiliza mafunzo hayo kwani ni msingi wa utekelezaji wa majukumu yao ya uwakilishi wa Wananchi.
Pia amewataka kujua mipaka ya kila MTU na kuepusha makundi ndani ya baraza kila mmoja atekeleze wajibu wake.
Mafunzo hayo yamewezeahwa na 1.TANARA MWENDA KUTOKA TAKUKURU
2. HALIMA MNENGE KUTOKA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA (TABORA)
3. ALPHONCE KASANYI KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA SHINYANGA
4. MARTINE MADALO KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA SHINYANGA
Baadhi ya picha za tukio hilo:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa