Maafisa Elimu Mji wa Kahama wafanya tathmini ya Umuhimu wa madarasa ya Utayari. Tathmini hiyo inafanywa kwa kupitia shule zote zenye vituo vya utayari na kuongea na walimu wa vituo hivyo, wazazi na viongozi wa maeneo husika.
Elimu ya utayari ni elimu inayotolewa kwa watoto wadogo ambao wamefikia hatua ya kujiunga na darasa la awali katika shule lakini wanashindwa kwasababu ya umbali. Hivyo kijiji au kitongoji kinaamua kumteua mwalimu wa kujitolea na kuwafundisha watoto hao katika eneo hilo kisha wakihitimu ndio wanaenda kujiunga na darasa la kwanza.
Akiwa katika timu hiyo ya tathmini Ndg. Sadick Kigaille ambaye ni Afisa Elimu vielelezo Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Mji Kahama amesema kuwa katika maeneo mengi wanaonesha uhitaji wa madarasa haya ya utayari. Amesema kuwa katika shule nyingi inaonesha kuwa watoto waliopitia madarasa ya utayari wanafanya vizuri wakiingia darasa la kwanza kuliko wanaoingia moja kwa moja.
Bw. Kigaille amebainisha kuwa wengi walioongea nao wanaongelea changamoto za kukosa miundombinu ya kufundishia kama vile maji, majengo ya kudumu n.k
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa