Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amewataka wananchi kujitoa kwa dhati katika kujenga maboma kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wapya. Ameyasema hayo Jana alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mahitaji ya vyumba vya madarasa kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi mapema mwakani kwenye kikao cha Kawaida cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Pili Julai - Septemba 2019 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
"Bado uhitaji ni Mkubwa sana, niwaombe tu Waheshimiwa Madiwani tuendelee kuhamasisha ujenzi wa maboma. Fedha za umaliziaji zipo zinasubiri maboma yakamilike. Tunajua hali sio nzuri lakini yote ni yetu na ni lazima vijana wetu wasome" Amesema Msumba.
Katika taarifa iliyowasilishwa kikaoni hapo inaonesha kuna upungufu wa Madarasa 577 ili kuweza kuwapokea wanafunzi wa madarasa ya awali na Msingi na vyumba 51 kwa Sekondari.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa