Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2017 Ndg. Amour Hamad Amour amesisitiza kuwepo kwa amani, Upendo, utulivu na Kujituma kuchapa kazi ili kuweza kufikia azma ya kuleta maendeleo.
Amesema haya leo akiwa Halmashauri ya Mji kahama wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru katika miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru. Pia kwa namna ya kipekee ameimwagia sifa Halmashauri ya Mji Kahama kwa kuweza kutekeleza sera ya viwanda kwa kutenga eneo kubwa la uwekezaji kata ya Zongomera.
Aidha kiongozi huyo amewaasa wananchi kutojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo hurudisha nyuma jitihada za maendeleo.
Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2017 ni “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu’’
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa