Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Ndg. Timothy Ndanya amewaasa viongozi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.
Amesema hayo mapema leo alipomuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama katika ufunguzi wa Mafunzo kwa Viongozi wa Umma kuhusu uzingatiaji na utekelezaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mafunzo hayo ambayo yamewezeshwa na wataalamu kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma - Kanda ya Magharibi yamehusisha viongozi wa Serikali kutoka sekta mbalimbali zilizopo Wilayani hapa.
Timu ya Wawezeshaji wa mafunzo hayo imeongozwa na Kaimu Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald Mwaitebele.
Akitoa neno la Shukrani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Mhe. Abel Shija Kishushu amesema kuwa fursa ya mafunzo kama haya ni vyema yakawa endelevu kwani yana nafasi kubwa katika utendaji wa viongozi wa Umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba ameahidi kuyasimamia yale yote yaliyoguswa na kuazimiwa kwenye mafunzo hayo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa