Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama wametoa elimu kwa wenyeviti wa Mitaa na Vijiji juu ya Utawala bora, amani na uwajibikaji. Hii imetokea Jumamosi ya Tarehe 20/05/2017 ambapo Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji walikuwa wanahitimisha mafunzo ya Mfumo Mpya wa Ruzuku za Maendeleo ulioboreshwa (Improved O&OD).
Akiongea kabla hajawakaribisha watoa mada alioambatana nao, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Ndg. Timothy Ndanya, alisisitiza juu ya Kuilinda amani ya nchi kwani ndo nguzo pekee inayowezesha maendeleo.
Mada zilizowasilishwa zilikuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Rushwa, uhamiaji haramu, Madawa ya Kulevya na utii wa Sheria.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa