Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeridhika na namna Halmashauri ya Manispaa ya Kahama inavyotekeleza Miradi yake ya Maendeleo.
Kamati hiyo imefanya ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi siku ya Jana Machi 17, 2025 ambapo imekagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Ujenzi wa Stendi Mpya ya Mabasi eneo la Mbulu na Soko la Sango, Ujenzi wa Mtaro wa Maji ya Mvua Shunu -Magobeko na Ujenzi wa Barabara eneo la Viwanda Zongomera.
Aidha Kamati imemtaka Mkandarasi wa Barabara Kuongeza kasi ili amalize ndani ya Muda aliopatiwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa