Timu ya Wataalamu ya Halmashauri ya Mji wa Kahama imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo mapya ya Hospitali ya Mji wa Kahama. Haya yamebainishwa wakati wa ziara ya wataalamu hao kwenye eneo la ujenzi iliyofanyika mapema leo.
Akiongea kwenye ziara hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa anafarijika kuona kasi iko vizuri.
"Kasi ni nzuri na niseme tu kuwa naamini mradi utakamilika ndani ya wakati kama mkataba unavyoelekeza, ni mradi ambao ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa ambapo kwa Hospitali yetu inapaswa kupokea wagonjwa miambili lakini kwasasa hospitali inapokea zaidi ya watu mia nane kwa siku" Amesema Msumba.
Mradi wa ujenzi wa majengo ya Hospitali unasimamiwa na Suma JKT kwa mkataba wa miezi 18 na unagharimu shilingi Bilioni 3.7.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa