Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki mapema leo amefanya ziara Halmashauri ya Mji wa Kahama na Kujionea shughuli na fursa za uwekezaji zinazotekelezwa na Mji huo.
Akiwa Kahama Kairuki ameweza kukutana na wajasiriamali wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Viwanda Bukondamoyo maarufu kama "Dodoma" na kuridhishwa na mpango wa Halamashauri wa kuwaweka wajasiriamali hao eneo moja na kuwawezesha.
Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na Halmashauri katika kuwawezesha watu wake kwa kuwapatia maeneo bure kunaiweka Kahama kuwa mfano wa kuigwa na Mikoa mingine.
Katika hatua nyinge Kairuki ameahidi kwenda kuisemea Kahama katika kufungua fursa za uwekezaji kwani anaiona kahama kubwa katika siku za usoni.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa