Serikali Wilayani Kahama imetoa taarifa ya uwepo wa Ugonjwa wa miguu na midomo unaoathiri mifugo jamii ya Ng'ombe. Haya yamebainishwa kwenye Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha mapema leo.
Kwenye taarifa hiyo Macha amesema kuwa ugonjwa huo umezuka kwenye kata za Chona, Chambo na Nyankende halmashauri ya Ushetu.
Hata hivyo taarifa hiyo inasema kuwa wataalamu wa mifugo kutoka ofisi ya kanda Mwanza wametembelea maeneo hayo na kuchukua sampuli kwa ajili ya vipimo vya maabara ili kujiridhisha na kuchukua hatua za kuudhibiti ugonjwa huo.
Wakati taraibu zingine zikiendelea wafugaji wa maeneo hayo wanashauriwa wasitoe mifugo yao nje ya maeneo ambayo hayakuathirika na wala kuingiza mifugo ndani ya maeneo hayo yaliyoathirika.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa