Halmashauri ya Mji wa Kahama imefunga Mkataba na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB DEVELOPMENT BANK LTD) wa Kiasi cha Tsh. 382,500,000/ kwa ajili ya Uwezeshwaji wa Kiufundi (Technical Assistance Agreement) katika Kuandaa Upembuzi yakinifu (Feasibility Study) , Scheme Design, Detailed Designs, Bill of Quantities, Business Plan na Tender Documents kwa ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Kisasa.
Mkataba huo umesainiwa Leo Jijini Dar es Salaam kwa pande zote mbili kuafikiana kulinda na kutekeleza yaliyomo kwenye Mkataba huo.
Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa kukamilika kwa Stendi hiyo kutasaidia kuongeza wigo wa kutoa huduma na pia ni chanzo Cha Mapato.
"Tunategemea sasa hadi Mwezi Februari maandalizi ya awali na March 2019 Ujenzi unaanza kwa kipindi cha miezi 10 kwahiyo tunatarajia Mwakani mwezi.Septemba 2019 Stendi itaanza kufanya kazi" Amesema Msumba
Stendi ya Kisasa ya Mabasi inatarajiwa kujengwa Eneo la Mbulu mjini Kahama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa