Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Ardhi cha Dar es salaam imeanza maandalizi ya kutengeneza mpango kabambe mji wa Kahama "Master Plan"
Akiongea na timu kutoka Chuo kikuu cha ardhi waliofika Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa ajili ya kuchukua taarifa za awali za maandalizi hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa Kahama inahitaji kupangwa ili kuwa mji wa Kisasa.
" Mwaka 1998 kwa kushirikiana na Uholanzi ilifanyika jitihada za kuwa na mpango kabambe shirikishi angalau kuwe na kitu lakini ikafeli, baada ya kufeli ukaja mpango wa "demarcation" na bahati mbaya sana na ndio ikawa chanzo cha hali iliyopo...sasa hivi hata mfumo wa Maji taka huwezi kuweka..kwahiyo mji wetu kwa kata kumi na moja umejengwa kweli lakini umejengwa kienyeji ila kwa kata tisa bado zipo "Virgin" bado ni mashamba. Hali halisi tunahitaji kuwa na mji rafiki ambao utakuwa na mahitaji sahihi". Amesema Msumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango miji amesema kuwa kwa hatua ya awali ya kutengeneza Mpango huo wameanza na hatua ya kuchukua takwimu muhimu ambazo zitawasaidia katika kuandaa mpango huo. Hivyo amewataka wananchi watakao bahatika kufikiwa na timu hiyo watoe ushirikiano wa karibu kwa wadodosaji hao.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa