Halmashauri ya Mji wa Kahama imeadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kwa kutoa mafunzo kwa watumishi na wadau wanaotekeleza afua za UKIMWI juu ya upimaji mpya wa Index. Upimaji wa Index ni Upimaji wa kumdodosa mtu aliyepima na kukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ili ataje watu wake anaoshirikiana nao ngono au kama ni mama mwenye watoto chini ya miaka 5 au kama anajidunga atataja anaojidunga nao na kuwatafuta na kuwapima. Ni upimaji unaotafuta mnyororo na kuufatilia na kuwaleta kwenye huduma ya upimaji.
wadau walioweza kushiriki kwenye Mafunzo hayo ni pamoja na JHPIEGO, KONGA, COMPASSION na REDCROSS.
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hufanyika Disemba 1, kila Mwaka.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "JAMII NI CHACHU YA MABADILIKO TUUNGANE KUPUNGUZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU".
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa