Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ndg. Ludovick James Nduhiye amesema kuwa Mji wa Kahama ni sehemu ya Kujifunza kutokana na Mipango, Mikakati na Maendeleo yanayoonekana. Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mjini hapa.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji ambao kwa nyakati tofauti hawakusita kusifia hatua za kimaendeleo zinazochukuliwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama huku wakitoa ahadi ya kuona namna ya kuunga mkono juhudi hizo. Viongozi hao wametembelea eneo la Viwanda Zongomera maarufu kama DODOMA, Nyashimbi na Chapulwa-Mwendakulima.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa