Halmashauri ya Mji Kahama imeanza ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Iyenze. Ujenzi huu umekuja baada ya Serikali kuona haja ya kutanua wigo wa utoaji wa huduma ambazo kwenye zahanati zinakosekana ikiwemo pamoja na Upasuaji na uongezaji wa damu hususani katika masuala mazima ya Uzazi na watoto.
Ujenzi huu unakadiriwa kugharimu fedha za kitanzania takribani Milioni Mia saba na Ishirini ikiwa ni fedha za wadau na serikali, ambapo Serikali ya Canada wamechangia Milioni mia tano pamoja na fedha kutoka Serikali kuu Milioni miambili na ishirini. Gharama hizi ni pamoja ununuzi wa vifaa na mahitaji yote ya kituo kuweza kufanya kazi. Ujenzi unahusisha pamoja na chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wajawazito, Maabara ya Kisasa na ukarabati wa nyumba ya watumishi
Ujenzi wa Kituo hiko unatarajiwa kukamilika kufikia Mwisho wa Mwezi wa Desemba, Mwaka huu wa 2017.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa