Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amelirudisha rasmi Serikalini eneo la Vumilia maarufu kama Soko la Mkulima Mjini Kahama ambalo limekuwa na mvutano wa miaka mingi
Ametoa kauli hiyo mapema leo katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu Mjini Kahama. Mhe. Waziri amesema kuwa eneo hilo ambalo lilikuwa linatumiwa na Ushirika lilishafutwa na Rais tangu mwaka 1995 na kubaki kuwa mali ya Serikali ,hivyo litabaki kuwa la serikali na litapangiwa matumizi na serikali. Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi amesitisha shughuli za ujenzi wa makazi katika eneo lenye mgogoro la Chuo cha ufundi Mwanva hadi hapo maelekezo yatakapoletwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa