Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewataka watoa huduma za afya kuzingatia uadilifu katika majukumu yao. Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akitoa neno kwenye kikao cha tathmini ya utoaji wa huduma za afya ya msingi katika jamii kati ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na wajumbe wa timu ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kimejadili afua zifuatazo:
i. Afya ya baba, mama na mtoto
ii. Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
iii. Bima ya afya hususan CHF Iliyoboreshwa
iv. Matumizi ya Mifumo ya bajeti na ya kukusanya mapato na matumizi
v. Huduma za Ustawi wa Jamii
Kwenye afua hizi washiriki wamegusia mafanikio, changamoto na mipango ya utatuzi wa changamoto.
Kikao hiki kimewezeshwa na taasisi ya "Boresha Afya" ya mkoani Shinyanga.
Baadhi ya picha za kikao hiko:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa