Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha mapema leo amekutana na wanafunzi wa kidato cha Sita ambao ndio wameripoti kwa siku ya kwanza kutoka walikokuwa kwenye likizo iliyotokana na changamoto ya ugonjwa wa COVID_19.
Akizungumza na wanafunzi hao Mhe. Macha amewataka kuzingatia kanuni zote za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo pamoja na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
"Tunamshukuru Mungu kwa Tanzania tukiongozwa na Jemadari wetu Rais John Magufuli tumefanikiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya Corona, na Kahama hadi leo hatuna kifo hata kimoja, lakini haimaanishi kuwa corona imeisha, bado tunapaswa kujihadhari" Amesema Macha
Katika hatua nyingine Mganga mkuu wa Hospitali ya Mji wa Kahama Dkt. Lucas Ngamtwa akishirikiana na Maafisa afya wa mji wa Kahama wametumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi na walimu wa shule hizo juu ya ugonjwa wa Corona na namna ya kujikinga nao.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa