Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii, CHF Iliyoboreshwa, inatarajiwa kufanya kazi nchi nzima baada ya kuonesha mafanikio kwa Mikoa mitatu ya Morogoro, Shinyanga na Dodoma. Haya yamebainishwa na Kiongozi wa Mradi wa HPSS Profesa Minoris Meshack wakati akifungua semina elekezi kwa Waratibu na Maafisa Tehama wa CHF ngazi ya Halmashauri tarehe 16.04.2018 kwenye ukumbi wa Morena Mkoani Dodoma.
"Tunawapongeza sana watendaji wa hii mikoa mitatu kwani wamefanya kazi kubwa ya kuifikisha CHF hapa ilipo, bila jitihada zao leo tusingekuwepo hapa kuongelea kuipeleka nchi nzima" Amesema Pof. Meshack.
CHF Iliyoboreshwa kwa Mikoa mingine inatarajiwa kuanza mapema Mwezi wa tano endapo mambo yataenda kama yalivyopangwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa