Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limeendesha Mafunzo Kwa Wajasiriamali Mjini Kahama. Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia jana Tarehe 30/07/2018 hadi leo 31/07/2018 kwenye ukumbi wa Hlmashauri ya Mji Kahama.
Mafunzo haya ambayo yamefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack yamekuja baada ya ahadi ya Mhe. Waziri Mkuu aliyoitoa alipofanya ziara yake ya Kikazi Mjini hapa ambapo aliahidi kuagiza baraza la uwezeshaji kuja kuendesha mafunzo kwa wajasiria mali wa mji huu.
Timu iliyokuja kutoa mafunzo iliongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mrs. Beng'i Issa.
Zaidi ya Wajasiriamali 200 wamepatiwa mafunzo hayo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa